SIRI imefichuka! Kumbe yule Dokta Dismas John Macha aliyenaswa kwa tuhuma za kujifanya daktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar, Jumanne wiki hii, ni fundi wa umeme wa nyumbani, Risasi Jumamosi linaianika.
Akizungumza na mwandishi wetu Jumatano wiki hii, mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu wa Jeshi la Polisi ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo, alisema kwa mujibu wa uchunguzi wao, ilibainika kwamba dokta huyo feki ni fundi umeme wa siku nyingi.
Afisa huyo alisema kuwa hadi sasa uchunguzi zaidi juu ya Macha unaendelea ili kujua mambo mengine yaliyojificha.
Hata hivyo, hakuweka wazi ni hatua gani ambayo anaweza kuchukuliwa na kusisitiza kuwa lile ni kosa kubwa kwani linahusisha afya na maisha ya watu.
Baadhi ya mambo ambayo tumeyabaini kuhusu huyu jamaa, ni kuwa kumbe ni fundi umeme wa nyumbani na alichokuwa akifanya Muhimbili ni kutaka kujipatia fedha kwa mkato japo tunaendelea kupeleleza kujua ni wapi alipata vifaa vya udaktari,” alisema na kuongeza:
Tuhuma kama hii ni nzito, inahusisha afya na maisha ya watu kwa jumla, taratibu zinaendelea kujua mengi sana juu ya huyu bwana.”
Macha ambaye anadaiwa kutafutwa na uongozi wa Muhimbili kwa muda mrefu, alikamatwa na kufikishwa kwenye kituo cha usalama cha Muhimbili (Muhas) kwa mahojiano zaidi ambapo habari zilidai alisema yeye ni daktari wa Mwananyamala ambaye alifika hapo kwa ajili ya kuangalia wagonjwa wake wa nje. 
 
Top