Dr. Cheni |
Star huyo wa filamu za Nipende Monalisa, Jesica na Majanga aliendelea kwa kusema " Majukumu yangu hasa ni kuhakikisha simu hii watu wanatambua uwepo wake. Matangazo na promotion zinapofanyika nitakuwa na shiriki kikamilifu kabisa. Wamenipa mkataba wa mwaka mmoja kwa sasa na swali lako la thamani ya mkataba wangu naomba niweke kapuni kwasasa, ila millardayo.com itakuwa ya kwanza kujua thamani yake muda wa kuweka wazi ukifika. Ninachoweza kukwambia hivi sasa ni bei tu ya simu hizi ambayo ni Tsh 250,000 tu"
Wasanii wengi wakiwemo wa filamu siku hizi wanaanza kufaidi umaarufu wao baada ya kampuni mbalimbali kuanza kufanya nao kazi katika matangazo ya bidhaa zao kama mabalozi, wiki iliyopita Yobnesh Yusuph(Batuli), Rose Ndauka, Slim Omar na Single Mtambalike(Richie) walisainishwa mkataba wa kuwa mabalozi wa wa soko la hisa la Dar es salaam/ Dar es salaam Stock Exchange(DSE), King Majuto na JB ni baadhi ya wasanii wengine wa filamu ambao nao wana mikataba na makampuni katika kutangaza huduma na bidhaa za makampuni hayo.