Arin Andrews (kulia) na mwandani wake Katie Hill
Nchini
Marekani, yenye watu waliojibadili jinsia, 'transgender' wapatao laki
tisa, vijana wawili kati yao wamependana kimapenzi na huenda wakaoana.
Kijana Arin Andrews alizaliwa katika jinsia ya kiume, wakati binti Katie Hill alizaliwa katika jinsia ya kike.
Hivi karibuni, Arin alifanyiwa upasuaji wa kuondoa matiti yake (mastectomy) na kuanza kutumia vichocheo

vya
hormone za kiume (testosterone) ili kujenga umbo la kiume kama
anavyoonekana kulia kwenye picha. Alipoulizwa ikiwa hakujali kuwa na
makovu kifuani mwake kwa ajili ya kuondoa matiti, alisema alikuwa radhi
aishi na makovu kuliko kubeba matiti.
Akizungumza na wanahabari wa INSIDE EDITION, Arin ambaye awali alitambulika kwa jina la Emerald, anasema asingeweza kufikia hapo ikiwa asingepata upendo na ushirikiano kutoka kwa mpenziwe, Katie ambaye anayeelewa fika yanayoendelea kwenye kichwa chake.
Katie ambaye awali alitambulika kwa jina la Lucas, sasa hunyoa miguu yake ili isiwe na vinyweleo vingi kama mwanaume, jambo ambalo anasema lilimkosesha raha kila mara alipojitizama kwenye kioo kwa kujiona mbaya na asiyevutia. Anasema siku moja alipochoshwa sana na mawazo, alisema leo ni leo, liwalo na liwe; Akamketisha kitako mama yake na kumwambia "Usiku wa leo nitajiua endapo hutanisaidia," na hapo ndiyo ukawa mwanzo wa kuanza taratibu za kufanyiwa upasuaji wa kujibadili jinsia.
Mwaka jana, wazazi wa watoto hao wawili waliwakutanisha, na hapo ndipo mapenzi baina yao yalipowaka.