Hivi karibuni zilienea habari za chini chini kuwa muigizaji wa filamu nchini maarufu kwa jina la Rayuu zikidai kuwa ametoa mimba kienyeji na sasa yuko kitandani angali akiuguza maumivu...
Habari hizo zilimfikia mpekuzi wetu wa kitengo maalumu cha UMBEA na kuamua kumtafuta Rayuu ili atoe ufafanuzi wa issue hiyo.
Katika utetezi wake, mrembo huyo alizikana taarifa hizo na kudai kuwa yeye hana historia ya kuchoropoa mimba..Kilichomfanya augue ni maradhi ya kawaida na si kutoa mimba.