Kwa majina naitwa XXXXX XXXXXX ni muajiriwa wa campuni ya African Barrick Gold Mine idara ya ulinzi katika mgodi wa BUZWAGI.
Nilipata
kuwa fahamu katika account yenu ya twitter kwani mie ni kati ya watu
nilio wafollow nikifahamika kama @XXXXXXX(twitter).
Kwanza napenda kutowa pongezi kwenu kwani mmetuabarisha mambo mengi ambayo tulikuwa hatu yafahamu ndani ya nchi na nje pia.
Ningependa mfahamu kuwa ABG inashikilia migodi mikubwa mi nne hapa Tanzania nayo ni Buzwagi uliyopo kahama,Bulyhulu uliyopo
Kahama kijiji cha kakola,Tullawaka na North Mara uliyopo Mara.Sasa mm ningependa kuongelea mgodi wa Buzwagi ambao ndiyo ninapo
fanyia
kazi.Ni miezi miwili ipite tangu walipo sema kuwa wanaendesha mgodi kwa
hasara ingawa ss tunaona toka mgodi ulipo anza hakuna
tofauti kwani tofali za dhahabu ni zile zile wanazochukuaga
kila week (12kila week).Hivyo wakubwa wa mgodi walitowa memo inayo sema
kuwa
kutakuwa na operation kifaru yaani wanaifananisha hali ya
kupunguza wafanyakazi kama mnyama faru.Cha ajabu kwetu ni kuhusu malipo
ya watakao
punguzwa kazini kwani wanadai kuwa mtu mwenye
mwaka mmoja kazini atalipwa mshahara wa mwezi mmoja tuu na mtu mwenye
miaka miwili kazini
atalipwa mishara ya miezi miwili tuu sasa
ss tunashangaa sana juu ya hali hiyo tena wanajidai na wanasema hiyo
wanatusaidia tuu.Dipartment zitakazo
punguzwa ni Mine,Site service,Maintenance,Safety, Community,na Process plant idara yangu mm haija guswa ila nimeona huruma ndiyo maana nikawapa
hizi habari pengine mtaweza kufwatilia na kujuwa sharia inatakaje maana wengi wanaonewa sana hapa Buzwagi.
Nihayo tuu kwa ufupi ila bado nakusanya habari na nitaedelea kuwahabarisha
jinsi huu mgodi unavyoendeshwa.