MSANII maarufu wa filamu hapa nchini, Jacqueline Wolper,
amewataka wasanii wenzake wa kike kuacha kuvaa nguo zisizo na maadili ya
Kitanzania kwa kuwa wao ni kioo cha jamii.
Wolper aliyasema hayo hivi karibuni wakati akihojiwa katika kipindi
cha Take One cha Clouds FM, baada ya kuibuka ‘staa’ mwenye muonekano
mzuri kuliko wasichana wote katika tasnia hiyo.
Alisema ana imani mashabiki wake wanamkubali licha ya kutovaa nguo zisizokuwa na maadili ya Kitanzania kama wasanii wenzake.
“Mimi nawakubali sana mashabiki wangu kwa kunipigia kura hadi kuibuka
mshindi na ni kweli, najiamini kwa kuwa mimi hata siku moja huwezi
kuniona nimevaa nguo za nusu uchi kama wengine,” alisema na kuongeza
kuwa anajiheshimu na hawezi kuvaa mavazi hayo.