From GLOBALPUBLISHER:
Stori: Brighton Masalu
SIKU chache baada ya kustaafu muziki, mwanamuziki mkongwe nchini, Maalim Mohamed Gurumo ‘Mzee Gurumo’ amekiri kupitia maisha mabaya ujanani ikiwemo kufumaniwa na mke wa mtu pamoja na uvutaji wa ‘sigara kubwa’ Ijumaa linaanika.

Akizungumza katika mahojiano na Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Runinga ya East Africa chini ya Mtangazaji, Salama Jabiri mwanzoni mwa wiki hii, Gurumo alisema miongoni mwa mambo mabaya ambayo hawezi kuyasahau maishani mwake ni pamoja na hayo.
KUFUMANIWA:
Katika sakata hilo, Gurumo alisema kuwa ilikuwa ni mwaka 1961 ambapo alikuwa na uhusiano na mke wa mtu ambaye aligoma kumtaja, ndipo siku moja wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo ‘wakiponda kirauli’ ghafla walisikia hodi na ndipo mwanamke huyo alipomwambia kuwa anayegonga mlango ni mumewe.
“Niliogopa sana, ikabidi nijibanze nyuma ya mlango, alipoingia tu...............

nikatimua mbio kali sana, lakini hakujua kama ni mimi,” alisema Gurumo.
Kuhusu uvutaji wa bangi, Gurumo alikiri kuwahi kuonja kilevi hicho ujanani mwake ambapo alibainisha kuwa alishawishiwa na mwimbaji mwenzake maarufu sana kwa wakati huo.
Alisema siku ambayo alivuta sigara kubwa, alipofika nyumbani baada ya kutengewa chakula, alimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa akidhani ni mchuzi.
“Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwangu, nilivuta kutokana na ushawishi, baada ya kufika nyumbani, wakati wa chakula nilimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa, nikasema mbona mchuzi hauna ladha nzuri, lakini baadaye nilijutia sana,” alisema Gurumo na kuongeza:
“Nimepitia maisha ambayo si mazuri sana ujanani, lakini yote hayo ni mapito na imebaki kama historia tu kwangu, namuomba Mungu anisamehe kwa hayo,” alisema Gurumo.
 
Top