Na Sakina Shabani
Msanii zilipendwa kwenye sanaa ya filamu Sintah amefanya madudu mengine baada ya kuandika habari ya uongozi na uchochozi na kukipakazia kituo cha redio time fm cha Jijini Dar kuwa kilishindwa kujipanga kwenye shoo yao iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye suala la ulinzi hadi kupelekea wasichana kubakwa na kuporwa mali zao.

Habari hiyo iliwashangaza waandaji wa tamasha hilo pamoja na jeshi la polisi Kanda ya Kinondoni ambalo lilikuwepo uwanjani usiku kucha wakingozwa na mkuu wa kituo cha Polisi Oysterbay Wilbrod Mtafungwa hadi asubuhi bila kushuhudia matukio mabaya.

Katika habari hiyo ya Sintah iliyokuwa inasema kuwa Wasichana wabakwa usiku kucha na wahuni kwenye shoo ya Azonto bila msadaa wowote jambo ambalo Jeshi la Polisi Kinondoni limekanusha vikali madai hayo huku ikisema kuwa hadi leo Jumanne hakuna taarifa yoyote kuhusiana na madai hayo ya Sintah.

Akiongea na Xdeejayz mmoja wa askari wa kituo cha Oysterbay ambae aligoma kutaja jina lake kwa madai kuwa yeye si msemaji alisema" Tumeshangazwa sana na taarifa ya Sintah aliyoiandika jana Jumatatu mapema kuwa kuna wasichana walibakwa usiku kucha hii habari naona ilikuwa na mlengwa wa kushoto kwa kuchafuliana habari hiyo haina ukweli wowote kwani hadi sasa sisi kama Polisi tuliopewa jukumu la kulinda wananchi ziku zile hatuna taarifa hizo" Alisema afande huyo

Hata hivyo jeshi hilo lilikuwa na mpango wa kuhitaji ushahidi wa vielelezo juu ya habari hiyo ambavyo Sintah angetakiwa kuviwakilisha polisi ili waweze kuwasaka wabakaji hao vinginevyo habari hiyo ingemletea matatizo Sintah kwani ni ya uchochezi na unafiki.

Siku ya shoo hiyo ya mwanamuziki Azonto toka nchini Ghana mwenye makazi yake nchini Uingereza ilikuwa na ulinzi mkali sana kulikuwa na Mbwa wa polisi 15, Polisi wasiopungua 90 wakiwemo wale wenye siraha ambao walikuwa wanazunguka viunga vya uwanja wa Ustawi wa Jamii.

Aidha baadhi ya mashabiki wengi walisema kuwa huenda Sintah bado ana hasira na kituo hicho cha redio times baada ya kupigwa chini kwenye kipindi alichokuwa anatangaza kutokana na kukosa sifa ya kuendesha kipindi hali iliyosababisha Sintah kuwawekea bifu.

Hata hivyo Sintah aliitoa haraka habari hiyo kwenye blog hiyo baada ya kutonywa na wasamalia wema kuwa ingemletea matatizo makubwa kwani kama hana ushahidi wa vielelezo ni heri akaitoa na mara moja alifanya hivyo.

Xdeejayz iliwasiliana na uongozi wa redio times lakini bahati mbaya simu zao zote zilikuwa bize kila walipopigiwa simu, hata hivyo Xdeejayz inawaahidi wasomaji wetu kuwa itamtafuta mkurugenzi wa kituo hivho Rehure Nyaulawa kuzungumzia suala hilo na kama kuna hatua zozote wameshaanza kuzichukua juu ya Blog hiyo kwa kuandika bahari hiyo ya uongo.
 
Top