Tukio hilo ambalo alilifanya bila kukusudia, lilitokea hivi karibuni katika Kijiji cha Machali B, mkoani Dodoma wakati alipokwenda kuchunguza tatizo la kukauka kwa maji katika bwawa lililopo kijijini hapo.
Akiwa mkoani humo, mtangazaji huyo aliongozana na jopo lake na ulipofika wakati wa kutaka kujua uhalisia wa tatizo la kukauka kwa maji, ndipo alipozama kwenye matope kwa bahati mbaya.
“Unajua kile kijiji wakazi wake wanalalamika sana kuhusiana na maji ambayo wanakunywa kwa vile bwawa hilo limekauka kabisa na kuna wakati wanachota matope matupu, inasikitisha,” alisema Kiria.
Alibainisha kuwa, alikanyaga sehemu zenye matope dimbwini hapo akiamini pamekauka ndipo alijikuta akizama miguu bila kupenda (tazama pichani anaosha miguu).
“Nilipojaribu kukanyaga nilijua ni sehemu kavu kumbe ni matope ya nguvu, nilikumbana nayo kwenye miguu yangu yote,” alisema.