Ajali mbaya imetokea asubuhi ya leo majira ya saa 2 kwenye barabara ya majita karibu na makazi ya mkuu wa mkoa wa Mara baada ya gari aina ya VX land cruser namba T 901 AHH kuigonga pikipiki iliyokuwa ikitoka maeneo ya mjini musoma kuelekea kamnyonge.
Kamera yetu imemshuhudia majeruhi wa ajali aliyedaiwa kuwa ni abiria akiwa anavuja damu nyingi kichwani huku akipumua kwa shida na muda mchache askari wa kikosi cha usalama barabarani walifika eneo la tukio na kumchukua kwa ajili ya kumuwahisha hospitali.
Mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo kabla ya camera ya blog hii kufika eneo la tukio muda mchache wamesema dereva wa pikipiki ambaye alidaiwa kupakia abilia alitaka kulipita gari hilo na kuingia eneo la gari hali iliyopelekea kutokea kwa ajali hiyo.
shommibinda blog