Video model Agness Gerald maarufu kama “Agness Masogange” ambaye ililipotiwa kwamba yeye pamoja na mdogo wake wamekamatwa nchini South Africa wakiwa na mzigo wa dawa za kulevya. Habari mpya hivi sasa ni kwamba wapo nje ya mikono ya polisi wa huko South Africa. Kutoka kwenye page za facebook na instagram za Agness Masogange zinathibisha hilo.
Page hizo ambazo hazikuwa updated tangu mwezi wa saba lakini usiku wa tarehe 17/9, Agness alikuwa anaandika status za shukrani kwa kuwa huru tena. Moja ya status inasomeka, “Thanks god nimeamini wewe ulikuwa pamoja na momo katika maombi yangu na thanks kwa wote mliokuwa mkiniombea, mungu kapokea maombi yenu”.
Status nyingine ambayo ilifuatana na hii inasomeka,”All praise and glory to the lord almighty I thank you for my freedom amen”. Hizo zote mbili zilikuwa kwenye facebook page yake. Kwenye instagram nako alipost picha yenye caption za “Thnxx god I knw u gud for me”.